Lugha Nyingine
Ethiopia yazalisha mapato ya mauzo ya nje ya dola milioni 14.5 kutoka eneo maalumu la viwanda lililojengwa na China
Meya wa Mji wa Dire Dawa Ahmed Mohamed Bouh akizungumza kwenye uzinduzi wa Eneo Maalumu la Viwanda la Shirika la Uhandisi na Ujenzi la China (CCECC) huko Dire Dawa, Ethiopia, Mei 28, 2021. (Xinhua)
ADDIS ABABA - Serikali ya Ethiopia imesema ilizalisha takriban dola za Kimarekani milioni 14.5 katika mapato ya mauzo ya nje kutoka kwenye bidhaa zinazozalishwa kwenye Eneo Maalumu la Viwanda la Dire Dawa lililojengwa na China katika mwaka wa fedha wa 2021/22 uliomalizika Julai 7.
Eneo la Viwanda la Dire Dawa, ambalo lilijengwa na Shirika la Uhandisi na Ujenzi la China (CCECC) na kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Mwaka 2020, lina jumla ya viwanda 15 vilivyojengwa ndani ya eneo hilo.
“Eneo hilo la viwanda lilizalisha mapato ya mauzo ya nje ya nchi yaliyoripotiwa kutoka kwa bidhaa kama vile viatu na bidhaa za nguo, miongoni mwa mengine,” Shirika la Habari la Serikali ya Ethiopia (ENA) lilimnukuu Kamil Ibrahim, mkuu wa Eneo Maalumu la Viwanda la Dire Dawa, akisema Jumamosi.
Kwa mujibu wa Ibrahim, masoko makuu ya mauzo ya bidhaa zinazozalishwa na makampuni yanayofanya kazi ndani ya Eneo Maalumu la Viwanda la Dire Dawa yanatajwa kuwa China, Pakistani, Marekani na Djibouti.
Siku ya Ijumaa, Wizara ya Biashara na Ushirikiano wa Kikanda ya Ethiopia ilisema nchi hiyo ilipata zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 4.12 kutokana na mapato ya mauzo ya nje katika mwaka wa fedha wa Ethiopia uliomalizika hivi majuzi.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilikuwa na lengo la awali la kuzalisha dola za kimarekani bilioni 4.63 kutokana na sekta ya mauzo ya nje. Dola hizo za Marekani bilioni 4.12 zilizoripotiwa zinaelezwa kuwa ongezeko la asilimia 13.81 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita ambapo dola za Kimarekani bilioni 3.62 zilipatikana.
Wizara hiyo ilisema sekta ya kilimo ilichangia takriban asilimia 72 ya mapato yote ya mauzo ya nje, wakati sekta ya madini, viwanda na nishati ya umeme ilichangia sehemu iliyobaki ya mapato ya nje kwa mwaka huo.
Bustani ya Wanyama ya Chongqing yawasaidia wanyama kuepuka joto
Watu wafuruhia hali ya hewa nzuri wakati wa majira ya joto kwenye sehemu ya Mto Wujiang, Chongqing
Bwawa la Sanmenxia la katikati mwa China laanza kufanya kazi ya Kuondoa tope la mchanga
Mandhari ya Ziwa Yamdrok katika Mji wa Shannan, Mkoa wa Tibet, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma