Lugha Nyingine
Mkataba wa Biashara huria kati ya Mauritius na China waleta fursa zaidi kwa uuzaji wa nje wa bidhaa za Mauritius
Ukiwa mkataba wa kwanza uliotiwa saini na China na nchi ya Afrika, mkataba wa biashara huria kati ya China na Mauritius ulifanya kazi kuanzia tarehe 1, Januari, 2021. Ofisa mtendaji mkuu wa Shirikisho la Viwanda vya Sukari la Mauritius Devesh Dukhira alipohojiwa na shirika la habari la China Xinhua siku ya karibuni alisema, mkataba wa biashara huria kati ya China na Mauritius ulioanza kufanya kazi utatoa fursa nyingi zaidi za uuzaji wa nje wa bidhaa za Mauritius, na ana matumaini makubwa kwa uuzaji wa sukari maalumu za Mauritius nchini China.
Dukhira alijulisha kuwa, “Sukari ya miwa ilikuwa nguzo ya uchumi wa Mauritius, na hivi sasa bado ni mazao muhimu ya kilimo ya Mauritius.” Alikumbuka kuwa, kabla ya kutekelezwa kwa mkataba huo wa biashara huria, aina za bidhaa za Mauritius zilizouzwa nchini China zilikuwa chache sana. Mwongo uliopita, bidhaa za Mauritius zilizouzwa kwa China zaidi zilikuwa sukari ya miwa, vipuri vya saa na maua mabichi. “Mkataba huo wa biashara huria ulifungua mlango wa uuzaji wa nje wa bidhaa mbalimbali za Mauritius zikiwemo pombe ya rum na vitambaa.”
Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, Dukhira alipokuwa mkurugenzi wa mambo ya soko wa Shirikisho la Viwanda vya Sukari la Mauritius aliona uwezekano wa maendeleo ya sukari ya nchi hiyo katika soko la China. Mkataba wa biashara huria kati ya China na Mauritius umepanga “mgao wa ushuru ” kwa sukari ya miwa ya Mauritius: kuongeza uagizaji wa sukari ya nchi hiyo kwa tani 5,000 kila mwaka kutoka tani 15,000 ya mwaka 2021 hadi tani 50,000 ifikapo mwaka 2028. Ndani ya mgao huo , ushuru wa sukari ya miwa ya Mauritius utapungua kutoka asilimia 50 hadi asilimia 15.
Dukhira alijulisha kuwa, mwaka 2021, uuzaji wa sukari maalumu wa Mauritius kwa China umeongezeka hadi tani 10,000, na umeongezeka kidhahiri ukilinganishwa na miaka iliyopita. Na pia alisema, katika kipindi kirefu cha siku za baadaye, mkazo wa uuzaji kwenye soko la China utawekwa katika soko la sukari maalumu ambayo ni ya hali ya juu na kusaidia afya zaidi na ina thamani kubwa ya nyongeza. Hivi sasa sukari maalumu ya Mauritius imeuzwa kwa nchi na maeneo 55, na Ulaya bado ni soko kuu zaidi. Lakini anakadiri kuwa nafasi ya soko la China itaendelea kuongezwa siku hadi siku . “Nina imani kuwa sukari maalumu itapata mustakabali mzuri katika soko la China.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma