Lugha Nyingine
Uchumi wa Marekani huenda ukadorora: CNBC
Mwanamke akinunua chakula kwenye lori la kuuzia chakula huko New York, Marekani, Mei 11, 2022. (Xinhua/Wang Ying)
NEW YORK - Televisheni ya CNBC Jumatatu wiki hii imeripoti kwamba hatari za uchumi wa Marekani kuangukia kwenye mdororo mwaka ujao ni zaidi ya asilimia 50.
"Uchumi wa Marekani unaweza kuingia kwenye mdororo wa kiufundi, unaofafanuliwa kama robo mbili mfululizo za ukuaji hasi, mara tu mwishoni mwa robo ya pili ya Mwaka 2022," CNBC imeripoti ikimnukuu Richard Kelly, mkuu wa mkakati wa kimataifa katika Dhamana za TD.
“Kupanda kwa bei ya gesi pamoja na Benki Kuu ya Marekani kuongeza riba na uchumi unaopungua kwa ujumla ni kati ya hatari za pande tatu zinazokabili nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi duniani hivi sasa,” Kelly amesema.
CNBC imeripoti ni ngumu kutabiri ni lini kudorora kwa uchumi kutaanza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma