Lugha Nyingine
Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya Hanzi--maandishi ya Kichina ” kwa Mwaka 2022 kuanza hivi karibuni
Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya Hanzi--Maandishi ya Kichina” kwa Mwaka 2022 yanayoandaliwa na Shirika la Urafiki wa watu wa China kwa nchi za nje (CPAFFC) na kuendeshwa na People's Daily Online, yataanza kote duniani mwezi huu wa Julai.
Kaulimbiu ya mwaka huu ya mashindano hayo ni "Yi" (義), hii ni dhana ya kifalsafa katika zama za kale nchini China, ambayo inamaanisha wema na haki katika ufafanuzi wa wasomi wa Confucius, na inamaanisha maadili na haki katika ufafanuzi wa wasomi wa Mohism.
Confucius, mwalimu mkuu, mwanafikra mkuu na pia mwanzilishi wa falsafa ya Confucius katika zama za kale nchini China, aliwahi kusema, "Mtu asiyefanya chochote anapokutana na dhuluma ni mwoga"; na Mencius, mwanafalsafa mwingine wa zama za kale za China katika shule ya mawazo ya Confucius, aliamini kwamba “Hisia ya aibu ndiyo mwanzo wa kutetea haki .”
Taratibu za Mashindano:
Mashindano hayo ya kimataifa yanajumuisha raundi za awali, nusu fainali na fainali. Rausi mbili za kwanza za mashindano hayo zitafanyika kwenye mtandao wa intaneti. Washiriki watajibu maswali na kutoa video ya dakika moja ya kujitambulisha katika raundi ya kwanza. Washiriki wa raundi ya pili watashiriki kwenye mashindano kwa njia ya video na kuongea kwa ufupi. Baada ya kujumlisha kura zilizopigwa na wataalamu na majaji, washindi 10 bora watakaochaguliwa wataingia kwenye fainali, ambazo zimepangwa kufanyika nje ya mtandao katikati hadi mwishoni mwa Mwezi Septemba.
Kila mshindi atatoa hotuba ya dakika saba kuhusu mada ya "Yi" (義) kwa Kichina, huku tuzo mbalimbali zikitarajiwa kuamuliwa kulingana na alama na maoni yatakayotolewa na majaji.
Sifa za wanaostahili kushiriki:
- Wanafunzi wa kigeni wanaosoma nchini China, wakiwemo wale wenye asili ya China ambao ni wahamiaji wa kizazi cha tatu;
- Raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini China ambao lugha yao ya asili si Kichina na ambao lugha ya asili ya wazazi wao si Kichina;
- Wazungumzaji wengine wasio na asili ya Lugha Kichina ambao siyo raia wa China.
Hakuna kikomo cha umri kwa washiriki.
Muhimu: Waliofuzu kwa raundi ya mwisho katika Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya Hanzi--Maandishi ya Kichina ” kwa Mwaka 2021 hawastahili kuingia nusu fainali na fainali kwa mashindano ya mwaka huu.
Ratiba ya mashindano:
Raundi za awali mtandaoni - washiriki watajibu maswali na kutoa video ya dakika moja ya kujitambulisha kuanzia Julai hadi Agosti mapema.
Nusu fainali ya mtandaoni - washindi wa nusu fainali watagawanywa katika vikundi ili kutoa hotuba mtandaoni zisizotarajiwa kupitia njia ya video mwezi Agosti. Washindi kumi bora watachaguliwa kushiriki katika raudi ya mwisho kulingana na alama zinakazotolewa na wataalam na waamuzi.
Fainali za nje ya mtandao – washindani wa fainali watatoa hotuba ya dakika saba inayolenga mada ya "Yi" kwa Kichina katikati hadi mwishoni mwa Septemba. Waamuzi watatoa alama kwa kila moja ya hotuba na kuchagua bingwa wa mwisho pamoja na wapokeaji wa tuzo mbalimbali kulingana na uwezo wa washiriki wa kuzungumza lugha ya Kichina, kujieleza, ujumbe wa msingi wa hadithi zao, na jinsi hadithi zao zinaweza kuhimiza mabadilishano kati ya ustaarabu tofauti.
Vidokezo:
Washiriki watatakiwa kujibu maswali matano ndani ya dakika 10 kupitia programu ndogo ya WeChat wakati wa duru za awali.
Baada ya kujibu maswali, washiriki wanapaswa kuandika neno la Kichina wanalopenda kulingana na maagizo yaliyotolewa.
Washiriki lazima watume video ya dakika moja ya kujitambulisha kupitia barua pepe ya: hanzi@people.cn kabla ya saa 6 usiku (Saa za za China) Agosti 5. Kichwa cha barua pepe yako lazima kitumie mpangilio ufuatalo: “jina lako + namba yako ya simu ya mkononi” (Kumbuka: jina na nambari ya simu inapaswa kuendana na zile zinazotumiwa wakati wa kujibu maswali).
Mahitaji au mfumo wa faili ya video: MP4, 1080P, mfumo wa upana. Video haipaswi kuwa zaidi ya dakika moja kwa urefu. Unaweza kutumia miunganisho na hadithi zozote za kibinafsi kati yako na Hanzi ya Kichina kwenye video yako).
Washiriki 30 bora watatinga nusu fainali kulingana na matokeo ya jumla watakayopata katika hatua ya awali.
Skani msimbo wa QR hapa chini ili kuanza kujibu maswali:
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma