久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

China na nchi za Caribbean zaimarisha ushirikiano wa kina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2022

JINAN - Kituo cha Maendeleo cha China na Caribbean Jumatano wiki hii kimezinduliwa huko Jinan, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, ambacho kinatarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya China na nchi za Caribbean.

Miradi mitatu ya ushirikiano kati ya China na nchi za Caribbean pia ilitangazwa, ambayo ni pamoja na uchangiaji wa vifaa tiba vya kupambana na janga la UVIKO-19 kwa nchi husika, ushirikiano na Guyana kuhusu mafunzo ya uvuvi wa baharini, na uzinduzi wa jukwaa la kimataifa la kupashana habari za mafanikio kuhusu maendeleo ya pamoja na watu katika eneo la Caribbean.

Picha iliyopigwa Tarehe 6 Julai 2022 ikionyesha hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Maendeleo cha China na Caribbean huko Jinan, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua)

Kustawi biashara

China na nchi za Caribbean zimeimarisha ushirikiano katika sekta nyingi, kati ya hizo zinazoonekana zaidi ni biashara.

"Kahawa ya Jamaika ya Mlima Bluu ni nzuri sana. Ndiyo nimekuwa nikitafuta,"yanasema maoni kwenye jukwaa la biashara ya mtandaoni la China la JD.com.

Kampuni ya Shanghai Inter-Ocean Enterprise ambayo ni wasambazaji wakuu wa kahawa hiyo ya Jamaica nchini China, imeshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya China ya Uuzaji na Uagizaji Bidhaa Nje (CIIE) kwa miaka minne mfululizo, imejitolea kueneza umaalumu wa kahawa hii ya Jamaika kwenye soko la China.

Picha iliyopigwa Novemba 6, 2018 ikionyesha bidhaa za kahawa za Mlima Bluu kwenye banda la Jamaika wakati wa Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya China ya Uuzaji na Uagizaji Bidhaa Nje (CIIE) huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

"Wakati wa CIIE ya pili, Jamaika ilikuwa mmoja wa wageni waheshimiwa. Kiasi cha mauzo yetu kwenye banda kilifikia yuan 300,000 (kama dola za Kimarekani 45,000)," anasema Xu Hao, afisa mkuu wa uendeshaji wa kampui hiyo.

Pia biashara kati ya China na nchi nyingine kutoka Caribbean ya Costa Rica hususani ile ya vitunguu saumu imeendelea kuchanua na kuleta faida kwa pande zote.

Wageni wakipita kwenye banda la Jamaika wakati wa Maonesho ya pili ya Kimataifa ya China ya Uuzaji na Uagizaji Bidhaa Nje (CIIE) huko Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 6, 2019. (Xinhua/Yin Gang)

Ushirikiano katika kupambana na janga la UVIKO-19

China na nchi za Caribbean zimehimiza ushirikiano katika sekta zaidi, ikiwemo mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi alisema mapema mwaka huu kwamba nchi za Caribbean ziliipatia China msaada mkubwa wakati mapambano ya China dhidi ya janga hilo yalikuwa katika kipindi kigumu zaidi.

“Baada ya kuzuka kwa janga hilo katika nchi za Caribbean, China pia imeziambia uzoefu wake katika kupambana na UVIKO-19 bila kuchoka, na kutoa shehena za chanjo na vifaa tiba vya kupambana na UVIKO-19 kwa nchi za Caribbean zenye uhusiano wa kidiplomasia na China.” Wang alisema wakati wa mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tisa za Caribbean uliofanyika kwa njia ya video.

Picha iliyopigwa Machi 18, 2020 ikionyesha eneo la mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao wa intaneti kuhusu kuzuia na kudhibiti janga la UVIKO-19 miongoni mwa wawakilishi kutoka China na Costa Rika huko San Jose, Costa Rika. (Picha na Esteban Dato/Xinhua)

Analisa Low, Balozi wa Trinidad na Tobago nchini China, anatarajia nchi hizo mbili kushirikiana katika sekta zaidi.

"Mashirika mengi makubwa ya kimataifa ya China yameanzisha matawi nchini Trinidad na Tobago," amesema Low, akiongeza kuwa Kituo cha Maendeleo cha China na Caribbean kinaweza kuwa na jukumu la kuwezesha ushirikiano wa kibiashara na pia mabadilishano ya kiufundi katika uhifadhi wa bahari na maendeleo ya uchumi wa bluu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>