Lugha Nyingine
Uchumi wa kidijitali wa China wakua kwa zaidi ya mara nne katika muongo uliopita
Mfanyakazi akikagua vifaa katika kituo cha data cha Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya China kilichoko Mkoa wa Guizhou, China Mei 24, 2022. (Xinhua/Ou Dongqu)
BEIJING – Takwimu rasmi za Serikali ya China zinaonesha kuwa uchumi wa kidijitali wa China ulishuhudia upanuzi wa haraka katika miaka ya hivi karibuni, huku thamani yake ikiongezeka kutoka yuan trilioni 11 (dola za Kimarekani trilioni 1.65) Mwaka 2012 hadi zaidi ya yuan trilioni 45 Mwaka 2021.
“Kiwango cha uchumi wa kidijitali katika Pato la Taifa la China (GDP) kilipanda kutoka asilimia 21.6 hadi asilimia 39.8 katika kipindi hicho,” kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Upashanaji wa Habari ya China.
China imeongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kidijitali. Kufikia mwisho wa Mei, China ilikuwa imejenga mtandao mkubwa zaidi na wa viwango vya juu vya kiteknolojia zaidi duniani wa mtandao, unaojumuisha miji ya ngazi ya wilaya yenye mitandao ya fiber-optic na kuwa na vituo milioni 1.7 vya msingi vya teknolojia ya 5G.
China pia imeharakisha uunganishaji wa data kubwa, kompyuta ya wingu na akili bandia na sekta kama vile nishati, matibabu, usafirishaji, elimu na kilimo.
Wizara hiyo imesema, Mwaka 2021, pato la ongezeko la thamani la viwanda muhimu vya utengenezaji bidhaa za kielektroniki za upashanaji wa habari liliongezeka kwa asilimia 15.7 kuliko Mwaka 2020, na kufikia rekodi ya juu katika muongo mmoja, wakati mapato ya huduma za programu na teknolojia ya habari pamoja na mtandao na huduma husika pia zilirekodi ukuaji wa tarakimu mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma