Lugha Nyingine
Mtaalamu wa Zambia asema maafikiano ya kimataifa ya kuhimiza maendeleo yana umuhimu mkubwa
Mwanauchumi wa Zambia Kampamba Shula amesema anakubaliana na maoni aliyoyatoa rais Xi Jinping wa China kuhusu kufikia maafikiano ya kimataifa ili kuhimiza maendeleo ya dunia.
Hivi karibuni, Rais Xi Jinping wa China aliendesha Mazungumzo ya ngazi ya juu ya maendeleo duniani hapa Beijing kwa njia ya mtandao, ambapo alitoa hotuba yenye kauli mbiu ya “kujenga uhusiano wa kiwenzi wenye ubora wa juu, na kujenga kwa pamoja zama mpya ya maendeleo ya dunia”.
Shula amesema, hivi sasa kuna masuala mbalimbali ya siasa ya kijiografia duniani na maslahi tofauti, hivyo maoni ya rais Xi ni kutoa wito wa kutatua tofauti kwa njia ya uwazi. Amesema maendeleo ya dunia yanategemea nchi mbalimbali zikubaliane kufikia maafikiano hayo, haswa kuendana na malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, ili kuzifanya nchi tofauti zishirikiane na kupata maendeleo ya pamoja.
Watu wa Afghanistan warudi nyumbani baada ya tetemeko kubwa la ardhi wakiona nyumba zilizoharibiwa
Mandhari ya Bwawa la Hifadhi ya Maji la Xiaxi huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
Shughuli za kumkumbu za Siku ya Wakimbizi Duniani zafanyika Kampala, Uganda
Bandari ya Victoria ya Hong Kong yaadhimisha siku ya kurudi China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma