Lugha Nyingine
Wizara ya Biashara ya China yasema Marekani kuondoa ushuru dhidi ya bidhaa za China kutanufaisha pande zote
BEIJING - Wizara ya Biashara ya China leo Alhamisi ilisema kwamba upande wa China daima unashikilia kuwa kuondolewa kwa ushuru wa nyongeza uliowekwa na Marekani dhidi ya bidhaa za China kutanufaisha nchi hizo mbili na Dunia.
Msemaji wa wizara hiyo Shu Jueting amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa kwa kuzingatia hali ya sasa ya kupanda kwa mfumuko wa bei, kadiri upande wa Marekani unavyoondoa ushuru wake wa nyongeza kwa bidhaa za China mapema zaidi, ndivyo wanunuzi bidhaa na wafanyabiashara wanavyonufaika haraka zaidi.
“Pande hizo mbili zinapaswa kukutana katikati na kufanya juhudi za pamoja ili kutengeneza hali na mazingira ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na kudumisha utulivu wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili na Dunia kwa ujumla,” Shu amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma