Lugha Nyingine
Xinjiang yashuhudia kuongezeka kwa biashara ya nje
URUMQI - Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang wa China umeshuhudia kuongezeka kwa biashara ya nje sanjari na kuongezeka kwa safari za treni za mizigo kati ya China na Ulaya, ujenzi na uendelezaji wa bandari za nchi kavu na maeneo maalumu ya kiuchumi yaliyounganishwa.
Mkoa huo umerekodi zaidi ya Yuan bilioni 67.4 (kama dola bilioni 10 za Kimarekani) katika biashara ya nje katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 30.9 mwaka hadi mwaka.
Idara ya Forodha ya Urumqi, ambao ni Mji mkuu wa mkoa huo, ilisema kuwa kuanzia Januari hadi Mei, eneo hilo lilifanya biashara na nchi na kanda 157.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, njia za reli za usafiri wa treni za mizigo kati ya China na Ulaya kupitia Bandari ya Alashankou ya Xinjiang zimefikia 80, zikitoka katika mikoa 24 ya China kwenda nchi 13 zikiwemo Ujerumani, Russia na Hungary.
Xinjiang inajivunia kuwa na bandari mbili kati ya bandari nne kubwa nchini China kwa huduma za usafiri wa treni za mizigo kati ya China na Ulaya.
Mwaka 2011, Bandari ya Alashankou ilishuhudia treni ya kwanza kama hiyo kuelekea Duisburg, Ujerumani. Miaka mitano baadaye, Bandari ya Horgos ilikaribisha treni yake ya kwanza ya mizigo kati ya China na Ulaya.
Kwa mujibu wa Shirika la Reli la Urumqi, tangu kufunguliwa kwa huduma za treni za mizigo kati ya China na Ulaya na China na Asia ya Kati, Bandari za Horgos na Alashankou zilirekodi usafiri wa mara 50,000 za treni za mizigo kati ya China na Ulaya. Mwaka 2021, treni za mizigo za kati ya China na Ulaya zilisafirisha bidhaa zenye uzito wa tani milioni 1.46 zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 74.9, ikichukua asilimia 8 ya jumla ya biashara kati ya China na Ulaya.
Xinjiang ina maeneo manne maalumu ya kiuchumi yaliyounganishwa katika maeneo ya Kashgar, Alashankou, Horgos na Urumqi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma