Lugha Nyingine
Makampuni ya kimataifa bado yanaichukulia China kama kimbilio muhimu
JINAN - Ingawa mnyororo wa ugavi wa kimataifa umeingia katika kufanyiwa muundo mpya, China bado ni kivutio muhimu cha uwekezaji kwa makampuni ya kimataifa duniani kote, inasema ripoti.
Ripoti hiyo imetolewa na Taasisi ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi ya China chini ya Wizara ya Biashara ya China kwenye Mkutano wa tatu wa Makampuni ya Kimataifa wa Qingdao uliofanyika Jumapili iliyopita katika mji wa pwani wa Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China.
“Wafanyabiashara wa kigeni wa viwanda vingi vya uzalishaji bidhaa nchini China bado wanaona China ni sehemu muhimu ya uwekezaji wao huku imani yao ya uwekezaji ikiongezeka kila mara,” inasema ripoti hiyo.
Ripoti inaeleza kuwa, pamoja na ufinyu wa uwekezaji wa kimataifa katika viwanda vya utengenezaji wa bidhaa katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikivutia uwekezaji wa kimataifa katika sekta ya viwanda kutokana na soko lake kubwa na mnyororo kamili wa usambazaji.
Inasema kuwa, kuanzia Mwaka 2017 hadi 2021, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini China (FDI) kwenye viwanda vya utengenezaji bidhaa ulibaki thabiti, wakati uwekezaji wa kimataifa katika sekta hiyo duniani ulikumbwa na msukosuko wa kupungua.
Viwanda vya utengenezaji wa bidhaa vya China vilitumia dola za kimarekani bilioni 33.73 za uwekezaji wa kigeni Mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.8 kuliko mwaka 2020. Ukuaji ulikuwa asilimia 1.1 zaidi ya ule wa sekta ya viwanda duniani.
Kampuni za kimataifa zinazowekeza kwenye viwanda vya utengenezaji bidhaa zimekuwa zikiongeza mnyororo wa thamani katika uwekezaji wao nchini China katika miaka ya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, viwanda vya utengenezaji bidhaa kwa teknolojia ya juu vya China kwa hakika vilitumia dola za kimarekani bilioni 12.06 za uwekezaji wa kigeni Mwaka 2021, kutoka dola bilioni 9.89 za Marekani Mwaka 2017. Kiwango chake katika sekta nzima ya viwanda kilipanda kwa asilimia 6.3 hadi asilimia 35.8.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma