Lugha Nyingine
China yasema ina matumaini ya kuweka biashara ya nje ndani ya viwango vinavyofaa Mwaka 2022
Picha iliyopigwa Mei 1, 2022 ikionyesha meli ya kontena ikitia nanga kwenye Kituo cha Kontena cha Qianwan huko Qingdao, Mkoa wa Shandong Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Ziheng)
BEIJING – Wizara ya Biashara ya China Alhamisi wiki hii imesema China ina uhakika wa kuweka biashara yake ya nje katika kiwango kinachokubalika kwa mwaka mzima, na kutoa mchango zaidi katika misingi ya kiuchumi.
Thamani ya jumla ya uuzaji wa bidhaa na uagizaji wa bidhaa kutoka nje nchini China ilipanda kwa asilimia 9.6 kuliko mwaka jana mwezi uliopita ikiwa ni kiasi cha juu kuzidi asilimia 0.1 ya Mwezi Aprili, na kupata kasi ya kufufuka.
"Kuimarika huko kumekuja wakati ambapo uzalishaji kwenye biashara za nje umekuwa kipaumbele na hatua za kuhimiza ukuaji wa uchumi zilianza kutekelezwa," Msemaji wa wizara hiyo Shu Jueting amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Akibainisha kuwa hali ya kutokuwa na uhakika kama vile kuimarika kwa uchumi wa Dunia na matatizo yanayohusiana na gharama, minyororo ya ugavi na uchukuzi bado yapo, Shu amesema kuwa uratibu madhubuti wa udhibiti wa janga la UVIKO, maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na hatua za kusaidia zitawezesha ukuaji wa biashara ya nje.
Kupunguza kodi na uwezeshaji wa biashara unaoletwa na mikataba ya biashara huria itakuwa na jukumu muhimu katika kukuza biashara ya nje, amesema Shu, akiongeza kuwa China ina kiasi kinachoongezeka cha washirika wa makubaliano ya biashara huria.
Mwezi mkubwa (supermoon) waangaza anga la usiku kote duniani
Ukuta Mkuu wa Milima Jinshan wa Chengde mkoani Hebei unaonekana kwenye mandhari nzuri ya mawingu
Wakulima wakivuna ngano ya majira ya baridi katika Kijiji cha Gaomiaoli, Shandong nchini China
Mandhari kando ya Mto Mergel Gol huko Hulun Buir, Mongolia ya Ndani nchini China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma