Lugha Nyingine
Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) nchini China waongezeka kwa asilimia 17.3 katika miezi mitano ya kwanza
Magari yaliyozalishwa yakihamishwa kupitia eneo la ofisi kwenye Kiwanda cha Magari cha Tiexi cha BMW Brilliance huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Februari 16, 2022. (Xinhua/Yang Qing)
BEIJING - Wizara ya Biashara ya China Jumanne wiki hii imesema kwamba, uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) katika China Bara, kwa matumizi halisi, uliongezeka kwa asilimia 17.3 kuliko mwaka jana hadi kufikia Yuan bilioni 564.2 katika kipindi cha miezi mitano ya kwanza ya Mwaka 2022.
Kwa viwango vya dola za Marekani, uwekezaji huo ulipanda kwa asilimia 22.6 kuliko mwaka jana hadi kufikia dola bilioni 87.77 za Marekani.
Takwimu za wizara hiyo zinaonesha kuwa, sekta ya huduma ilishuhudia mapato ya FDI yakiongezeka kwa asilimia 10.8 kuliko mwaka jana hadi kufikia Yuan bilioni 423.3, wakati ile ya viwanda vya teknolojia ya juu iliongezeka kwa asilimia 42.7 kutoka mwaka uliopita.
Takwimu hizo zinaonesha zaidi kwamba, hasa, FDI katika viwanda vya teknolojia ya juu ilipanda kwa asilimia 32.9 kutoka kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita, wakati ile katika sekta ya huduma za teknolojia ya juu iliongezeka kwa asilimia 45.4 mwaka hadi mwaka.
Katika kipindi hicho, uwekezaji kutoka Jamhuri ya Korea, Marekani na Ujerumani ulipanda kwa asilimia 52.8, asilimia 27.1 na asilimia 21.4 mtawalia.
Katika kipindi cha Januari hadi Mei, FDI iliyoingia kwenye eneo la Kanda ya Kati ya China iliripoti ongezeko la kasi la mwaka baada ya mwaka la asilimia 35.6, likifuatiwa na asilimia 17.9 katika eneo la Kanda ya Magharibi, na asilimia 16.1 katika eneo la Kanda ya Mashariki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma