Lugha Nyingine
Mwelekeo mpya wapeleka biashara za rejareja kwenye ukuaji chini ya maambukizi ya UVIKO-19
Watu wakijistarehe kwenye kituo cha kambi huko Chongqing, Juni 4. (Picha/ChinaDaily)
Ingawa maambukizi ya virusi vya korona yameleta shinikizo kwa matumizi ya wanunuzi, lakini mwelekeo mpya unaonekana unapeleka baadhi ya masoko kwenye ukuaji.
Mwelekeo huo unaonekana katika ustadi wa kupanda mimea kwenye roshani, kupiga kambi za hali ya juu, na ongezeko la uuzaji wa vyombo vya umeme vya akili bandia nyumbani.
Kwa kuwa hatua za kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona zinaweka ukomo juu ya safari ndefu, hivyo kupiga kambi kwenyevitongji kumekuwa shughuli mpya ya kuvutia watu. Wasafiri vijana wanatamani kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kupiga kambi, ambapo wanaweza kuchoma nyama na kupata vyakula mbalimali, kushiriki sherehe ya moto usiku, kupiga fashifashi na kupiga picha.
Katika kipindi cha sikukuu ya Duanwu ya jadi ya China mwanzoni Juni, gharama ya kukodi zana na vifaa vya kupiga kambi iliongezeka kwa zaidi ya mara moja ikilinganishwa na wakati kama huo wa mwaka jana. Shirika la Qunar, shirika la mtandao la safari ambalo makao makuu yake yako Beijing lilisema, kutumia magari ya mapumziko (RV) kumekuwa wimbi jipya pia.
Programu za kufanya mazoezi ya kujenga afya kwenye simu ya mkononi pia zinatumika zaidi nchini China. Wataalamu wanasema, watu wanapenda zaidi kufanya mazoezi ya kujenga afya kwa kufuata video au madarasa ya mubashara, hasa kwa kuwa wanakaa nyumbani kwa muda mrefu zaidi.
Ustadi wa kupanda mimea kwenye roshani pia unavutia wakazi wengi zaidi wa mjini, ukiwa umekuwa njia ya kupunguza shinikizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma