Lugha Nyingine
Wawekezaji wa kigeni wanunua hisa na dhamana nchini China, wakiwa na matarajio ya muda mrefu
Magari yakiendeshwa katika sehemu ya kiini cha biashara (CBD) katika eneo la Chaoyang la Beijing, Mji Mkuu wa China, Juni 6, 2022. (Xinhua/Ju Huanzong)
BEIJING - Wawekezaji wa kigeni waliendelea kuongeza uwekezaji wao katika hisa na dhamana za China, wakitoa turufu ya imani katika maendeleo ya muda mrefu ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa kifuatilia soko cha Wind, hadi kufikia Juni 10, soko la hisa la China lilikuwa limeshuhudia ongezeko la mapato halisi ya mtaji wa kigeni kwa siku kumi mfululizo za biashara zilizopita, ikiwa ni kipindi kirefu zaidi cha mapato halisi kufikia sasa mwaka huu.
Takwimu za Wind zinaonesha kuwa, wiki iliyopita, wawekezaji wa ng'ambo walitumia yuan bilioni 36.83 (kama dola bilioni 5.48 za Kimarekani) kwa hisa fulani za China kupitia hisa za soko la Hong Kong zilizouzwa kwenye sehemu za China bara, na kufanya kuwa ongezeko kubwa zaidi la wiki tangu mwanzo wa mwaka.
Idadi hiyo ilikuwa tofauti kabisa na utokaji wa jumla wa yuan bilioni 45.1 mnamo Machi, wakati ambapo kuibuka tena kwa UVIKO-19 kuliathiri uchumi wa China.
"Uwekezaji wa kigeni katika soko la fedha la China ulipata mabadiliko machache sana mwaka huu," anasema Monica Li, Mkurugenzi wa hisa wa Fidelity International. Kampuni hiyo sasa inamiliki karibu dola bilioni 6 za Kimarekani katika hisa daraja A.
Amehusisha uingiaji huo wa mtaji na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na athari ya mgogoro kati ya Russia na Ukraine, kupanda kwa viwango vya riba vya Benki Kuu ya Marekani na kuibuka tena kwa mara kwa mara kwa maambukizi ya UVIKO-19 nchini China.
Lakini wakati nchi ya China ambayo ni yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani iliporekebisha vizuizi kutokana na UVIKO mwishoni mwa Mei na kuchukua juhudi za kuongeza uzalishaji wa kiuchumi, soko la kifedha liliongezeka polepole.
China ilichukua hatua 33 za kina za kuleta utulivu wa uchumi wake mwezi uliopita na Baraza la Serikali la China liliamuru idara za serikali kuanzisha hatua za vitendo.
Fedha muhimu za kigeni zimekimbilia katika soko la fedha la China wakati huo. Mnamo Mei 20, uingiaji wa mtaji wa kigeni kwenye soko la hisa la China ulifikia yuan bilioni 14.24, na Mei 31, idadi hiyo ilifikia yuan bilioni 13.87, ambayo ni mapato mawili makubwa zaidi ya mwaka.
"Ndani ya wiki mbili tu Mwezi Juni, tumeona wawekezaji wa kigeni wakirundika ununuzi wao wa hisa za daraja A za China, na uingiaji wake ukipita jumla ya Mwezi Mei," amesema Li. "Hiyo inaonyesha mabadiliko makali na ya haraka ya hisia za soko."
Li anaamini kuwa soko la fedha la China litaendelea kuwa la kuvutia kwa mitaji ya kigeni katika muda mrefu, kwa kuzingatia misingi mizuri ya kiuchumi ya nchi ya China. Zaidi ya hayo, uwekezaji nchini China bado una nguvu ya kuvutia, kwani China inatoa malipo mengi ya hatari za kibiashara, ambayo yanasaidia kukabiliana na hali ya kuongezeka kwa kutokuwa na uhakika wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma