Lugha Nyingine
Misri yawatunuku wajasiriamali na kampuni ya biashara
Watu wakihudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo ya Mjasiriamali wa Misri (EEA) huko Cairo, Misri, Juni 11, 2022. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Mashindano ya Tuzo ya Mjasiriamali wa Misri (EEA), yaliyolenga kuangazia watu wenye uwerevu zaidi nchini humo, yalimalizika usiku wa Jumamosi iliyopita na kutangaza washindi wa awamu ya pili.
Waandaji walisema kuwa mashindano hayo yalifanyika kuanzia Machi 26, ambayo yalilenga zaidi kusifu watu wanaothubutu kufanya ujasiri, mageuzi na uvumbuzi , pamoja na watu walioanzisha shughuli zinazoleta hamasa kwa watu wa jamii.
Mwanzilishi wa tuzo hili (EEA), Amr Mansi, aliwaambia waandishi wa habari wa Xinhua kwenye hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika usiku wa Jumamosi iliyopita usiku karibu na Great Pyramids kwamba lengo kuu la hafla hiyo ni kuwapongeza watu wanaochagia uchumi wa hivi leo na kuwatia moyo watu wa vizazi vijavyo.
Alisema kuwa “watu hawa wana uwezo wa kufanya uvumbuzi na kufanya mafanikio katika kila kazi wanayofanya, ni mfano wa kuigwa kwa wengine, na kwa hivyo wanastahili kutambuliwa."
Mashindano hayo yameshuhudia mamia ya wajasiriamali katika sekta zaidi ya 17 kujiandikisha, na wagombea 91 waliteuliwa kushiriki kwenye mashindano ya mwisho.
Watu wakihudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo ya Mjasiriamali wa Misri (EEA) huko Cairo, Misri, Juni 11, 2022. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Watu wakihudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo ya Mjasiriamali wa Misri (EEA) huko Cairo, Misri, Juni 11, 2022. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma