久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Sekta ya Uchukuzi ya China yaboreshwa chini ya usimamizi wa Serikali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2022

Wafanyakazi wakisafirisha vifurushi vya bidhaa katika kituo cha utoaji na usafirishaji bidhaa huko Zhengzhou, Mkoa wa Henan Novemba 11, 2021. (Xinhua/Zhang Haoran)

BEIJING - Sekta ya Uchukuzi nchini China, inayoyumbayumba kutokana na janga la muda mrefu la UVIKO-19, inatazamia kuimarika tena huku sera za Serikali zinazounga mkono zikianza kutekelezwa hatua kwa hatua na sera kadhaa nzuri zaidi zikitungwa.

Fahirisi ya utendaji wa sekta ya uchukuzi nchini China, ambayo hufuatilia kiasi cha biashara, oda mpya, ajira, mauzo yatokanayo na sekta, na viwango vya matumizi ya vifaa katika sekta hiyo, ilikuwa asilimia 49.3 mwezi uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.5 kuliko mwezi uliopita, takwimu kutoka Shirikisho la Uchukuzi na Manunuzi la China (CFLP) zilionyesha.

Shikisho hilo limesema, katika kipindi hicho, kiwango cha uhifadhi wa bidhaa kwenye maghala nchini China kinaonesha upanuzi wa asilimia 50.2.

Uchukuzi katika biashara ya mtandaoni pia ulishuhudia kufufuka kwa biashara Mwezi Mei, huku upanuzi huo ukipanda pointi 2.1 hadi pointi 104.3 kuanzia Aprili.

He Hui, Msaidizi wa Mkuu wa CFLP, amehusisha mafanikio hayo yaliyotajwa hapo juu na hatua za China za kuboresha sekta ya uchukuzi na kusaidia biashara wakati huu wa changamoto, akisema kuwa sekta hiyo itashuhudia upanuzi zaidi Mwezi Juni.

China imetunga na kuanzisha sera nyingi kama vile kuondoa vizuizi katika usafirishaji na kupunguza mzigo kwa makampuni yanayofanya biashara ya uchukuzi ili kuimarisha mtiririko wa bidhaa muhimu.

Shanghai, ambayo ilikuwa imeathiriwa zaidi na virusi vya Korona, ilianzisha mpango wa utekelezaji wa kuharakisha ufufukaji wa uchumi mwezi uliopita, ikichukua hatua kama vile kuleta utulivu kwenye minyororo ya viwanda na ugavi katika Delta ya Mto Changjiang , na kurahisisha njia za ndani na kimataifa za uchukuzi na usafirishaji.

Mji huo ulishughulikia wastani wa jumla ya kila siku wa vifurushi milioni 11 vya utoaji wa haraka wa bidhaa mnamo Juni 1, siku ya kwanza ya kurejea kwa shughuli na maisha ya kawaida baada ya miezi miwili ya usimamizi uliofungwa ili kudhibiti kuibuka tena kwa UVIKO-19.

Miji mbalimbali ikiwa ni pamoja na Beijing imeanzisha utaratibu wa "orodha nyeupe" ili kufikia uwezo wa utoaji na usambazaji wa bidhaa na kusaidia kuanzishwa tena kwa utendaji kazi kwenye makampuni muhimu.

Usaidizi wa kifedha umetekelezwa kwa makampuni yanayofanya biashara ya uchukuzi kote nchini China ili kukabiliana na matatizo.

Benki ya Viwanda na Biashara ya China, Tawi la Shandong imetoa mikopo ya zaidi ya yuan milioni 800 (kama dola za kimarekani bilioni 1.19) kwa ajili ya kusaidia sekta ya usafirishaji na mikopo iliyotolewa na Benki ya Kilimo ya China, Tawi la Zhejiang kwa ajili ya makampuni ya mawasiliano na uchukuzi ilizidi yuan bilioni 3.53.

Hivi karibuni China ilisisitiza kurahisisha zaidi uchukuzi na usambazaji wa bidhaa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha uendeshaji wa wadau wa soko na kuleta utulivu wa uchumi.

Alipokuwa akikagua Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China siku ya Jumatatu wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang aliziagiza serikali za mitaa kuimarisha uratibu juu ya kuwezesha urahisi katika usafirishaji wa bidhaa kwa viwanda muhimu, maeneo na makampuni ya biashara, na kusaidia haraka iwezekanavyo kuongezeka zaidi kwa kiasi cha mizigo inayosafirishwa.

“Jitihada zaidi zinapaswa kufanywa ili kukuza wadau wa soko katika sekta ya uchukuzi na kuwasaidia kustawi wakati wa kujenga mfumo wa munganiko wa mawasiliano na uchukuzi ili kupunguza gharama za usafirishaji”, alisema Li.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>