久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Biashara ya nje ya China yaimarika tena huku kukiwa na kasi kubwa ya kufufuka kwa uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 10, 2022

BEIJING - Biashara ya nje ya China iliongezeka tena Mwezi Mei, ikiwa ni ishara njema ya kufufuka kwa uchumi kwa ujumla wake huku mfululizo wa sera za serikali za kuleta utulivu kwenye uchumi wakati kukiwa na kuibuka tena kwa UVIKO-19 zikianza kuzaa matunda.

Takwimu rasmi za Serikali ya China zilizotolewa Alhamisi wiki hii zinaonesha kuwa, thamani ya jumla ya uingizaji na uagizaji wa bidhaa ndani na nje ya China ilipanda kwa asilimia 9.6 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho hadi kufikia yuan trilioni 3.45 mwezi uliopita, ikiwa ni juu ya ongezeko la Mwezi Aprili la asilimia 0.1.

Kwa mujibu wa Idara ya Forodha ya China (GAC), katika miezi mitano ya kwanza ya Mwaka 2022, biashara ya nje ya China iliongezeka kwa asilimia 8.3 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho na kufikia yuan trilioni 16.04, hivyo kuzidi ongezeko la asilimia 7.9 katika kipindi cha Januari-Aprili.

Kwa kutazama hali ya dunia na dola za Marekani, thamani ya jumla ya biashara ya nje ya China ilifikia dola za Marekani trilioni 2.51 katika kipindi cha miezi mitano, ikiwa ni ongezeko la 10.3 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho.

Picha iliyopigwa Tarehe 21 Mei, 2022 kutoka juu ikionyesha treni ya mizigo ya China-Laos ikiondoka kwenye stesheni katika Mji wa Chongqing nchini China. (Xinhua/Tang Yi)

Takwimu za forodha zinaonesha kwamba, katika miezi mitano ya kwanza, mauzo ya nje ya bidhaa yalifikia asilimia 11.4 mwaka hadi mwaka huku uagizaji wa bidhaa kutoka nje ukiongezeka kwa asilimia 4.7, na kusababisha ziada ya biashara ya yuan trilioni 1.84.

Katika kipindi hiki, biashara kati ya China na washirika wake wakuu watatu wa kibiashara – Jumuiya ya nchi za Kusini-Mashariki ya Asia (ASEAN), Umoja wa Ulaya (EU), na Marekani -- iliongezeka kwa asilimia 8.1, asilimia 7, na asilimia 10.1 kutoka mwaka mmoja uliopita, mtawalia.

Wafanyakazi wakitengeneza nguo za kuuza nje kweye kampuni iliyoko eneo la Taihe, Mkoa wa Anhui nchini China, Mei 26, 2022. (Picha na Liang Xiaopeng/Xinhua)

Uungaji mkono wa kisera wazaa matunda

Katika kukabiliana na athari za kiuchumi zilizosababishwa na maambukizi ya virusi vya korona, Baraza la Serikali la China mwezi uliopita lilitoa mwongozo ukilenga kuboresha huduma na kutoa msaada zaidi wa kibajeti na kifedha kwa makampuni ya China yanayofanya biashara ya nje. Mwongozo huo ulifuatiwa na sera za kina za idara 27 za serikali.

Hatua hizi zililenga zaidi katika kurahisisha utaratibu wa biashara ya nje, kuimarisha msaada wa kifedha kwa makampuni ya biashara ya nje, na kuleta utulivu wa minyororo ya viwanda na ugavi kwenye biashara ya nje.

Picha iliyopigwa Mei 1, 2022 ikionyesha meli ya makontena ikitia nanga kwenye Gati la Makontena la Qianwan huko Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Ziheng)

Kufufuka kwa kasi kwa uchumi kuko njiani

Takwimu hizo za biashara za Mwezi Mei pia zinaongeza ushahidi unaoonyesha kuwa uchumi wa China unatikisa hatua kwa hatua athari za maambuziki ya virusi vya korona na hivyo kuleta kufufuka kwa kasi kwa uchumi.

Katika Taarifa yake ya hivi punde kuhusu Uchumi wa China iliyotolewa Jumatano wiki hii, Benki ya Dunia ilisema kwamba ikisaidiwa na vichocheo vya sera zake za kupunguza mdororo wa uchumi, kasi ya ukuaji wa uchumi wa China inatarajiwa kuongezeka tena katika nusu ya pili ya mwaka huu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>