Lugha Nyingine
China yaweka kipaumbele kwenye uthabiti wa minyororo ya viwanda na ugavi katika kustawisha uchumi wa viwanda
Wafanyakazi wakiwa wanashughulika kwenye karakana ya Kampuni ya vifaa vya kuzalisha umeme kwa upepo ya Harbin ya Kampuni ya Vifaa vya kielektroniki ya Harbin huko Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Mei 7, 2022. (Xinhua/Wang Jianwei)
BEIJING - China itaweka mkazo mkubwa zaidi katika kuhakikisha thabiti ya minyororo yake ya viwanda na ugavi kuwa, kwani inatazamia kustawisha tena uchumi wake wa viwanda baada ya kuzuka kwa UVIKO-19 katika miezi ya hivi karibuni.
Sekta ya viwanda ndiyo uti wa mgongo na injini ya ukuaji wa uchumi wa China, imesema Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Upashanaji Habari ya China (MIIT) katika mkutano wa hivi karibuni kwa njia ya video juu ya kukuza uchumi wa viwanda. Imeazimia kutoa nguvu kubwa zaidi za utekelezaji wa sera ili kuhakikisha upanuzi wa kuridhisha katika sekta ya viwanda katika robo ya pili ya mwaka huu.
Takwimu rasmi za hivi majuzi zilionyesha ukuaji wa polepole wa faida za makampuni makubwa ya viwanda ya China. Makampuni hayo, ambayo kila moja imekuwa na mapato yatokanayo na biashara ya kila mwaka ya angalau yuan milioni 20 (kama dola za Kimarekani milioni 2.98), yalishuhudia faida yao ikiongezeka kwa asilimia 3.5 ikilinganishwa na mwaka 2021 katika miezi minne ya kwanza ya Mwaka 2022, ikiwa ni tofauti kubwa na ukuaji wa asilimia 8.5 ya miezi mitatu ya robo ya kwanza.
Uchumi wa viwanda wa China bila shaka ulipata pigo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kwani mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Korona aina ya Omicron umelazimisha viwanda katika miji mikubwa kama vile Shanghai na Shenzhen na eneo lenye viwanda vizito katika Mkoa wa Jilin kusimamisha uzalishaji. Kuanzia viwanda vya kutengeneza semiconductors za hali ya juu, vipuri vya magari, na vifaa vya kielektroniki hadi viwanda vya nguo, shughuli za viwandani zilitatizwa katika nyanja tofauti. Vizuizi vya uchukuzi wa bidhaa viliibuka katika kipindi hicho.
China imechukua hatua za haraka ili kulainisha minyororo ya usafirishaji na uchukuzi wa bidhaa na kuchukua hatua kadhaa, kama vile mbinu ya "orodha nyeupe", kusaidia biashara katika maeneo yaliyoathiriwa na maambukizi ya virusi vya Korona kuanza tena uzalishaji na kuhakikisha usambazaji wa vipuri muhimu, vifaa na bidhaa.
Kampuni mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa zikiwemo za utengenezaji wa bidhaa kama vile nguo, simu za mikononi, vipuri vya magari, bidhaa za kielektroniki na kadhalika zimeanza kushuhudia wafanyakazi wakirudi kazini baada ya siku nyingi za kusimamishwa kwa uzalishaji.
"Tunapaswa kuweka mkazo mkubwa zaidi katika kuhakikisha uendeshaji mzuri kwenye minyororo ya viwanda na ugavi ili kustawisha uchumi wa viwanda," Waziri wa viwanda na upashanaji wa habari Xiao Yaqing alisema. Alisisitiza kuwa wizara yake itahakikisha utendakazi thabiti wa minyororo hiyo katika viwanda muhimu, biashara muhimu na sehemu muhimu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma