Lugha Nyingine
Pilikapilika ya manunuzi ya mtandaoni ya katikati mwa mwaka nchini China yachangia ufufukaji wa matumizi
Wafanyakazi wakisafirisha mizigo ya vifurushi kwenye kituo cha usafirishaji huko Zhengzhou, Mkoa wa Henan wa katikati mwa China, Novemba 11, 2021. (Picha/Xinhua)
Shughuli za manunuzi kwenye mtandao wa internet katikati ya mwaka nchini China ambazo zitafanyika kwa wiki kadhaa zilianza kwa hatua madhubuti katika wakati wa ufufukaji wa biashara na utekelezaji wa sera za kuhimiza ukuaji wa uchumi. Wachambuzi wanasema kuwa, kutokana na kupungua kwa athari za UVIKO-19, shughuli hizo zitachangia kustawisha uchumi.
Shughuli za manunuzi za kila mwaka zinaanzia tarehe 1, Juni, ambapo shughuli nyingi za kuhimiza manunuzi zilifanyika kwenye majukwaa mbalimbali ya biashara ya mtandao ya intaneti.
Katika masaa manne ya mwanzo ya shughuli za kuhimiza manunuzi ya JD.com, uuzaji wa jumla wa televisheni ya michezo yalizidi yale ya mwezi wa Juni wa mwaka jana, huku uuzaji wa simu za mikononi za chapa sita kuu zenye bei ya zaidi ya Yuan 4000 (Dola za Marekani 596 hivi) ukiongezeka kwa mara dufu ukilinganishwa na mwezi huu wa mwaka jana.
Kutokana na China kuharakisha kutekeleza sera za kutuliza uchumi, ufufukaji wa biashara za rejareja umechangia ongezeko kubwa la uchumi. Kwa mfano, baada ya miezi miwili ya usimamizi na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona kwenye maeneo ya makazi, Shanghai ilishughulikia vifurushi milioni 11 tarehe 1, Juni, ambavyo ni siku ya kwanza ya kurudia kwenye hali ya kawaida ya uzalishaji na maisha kwa mji huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma