Lugha Nyingine
China yazitoa sera na hatua za kusaidia uchumi
Picha iliyopigwa kutokea angani Tarehe 5 Mei 2022 ikionyesha eneo la ujenzi wa Makutano ya Bandari ya Gaolan ya Mradi wa Awamu ya Pili ya Barabara Kuu ya Hezhou-Gaolan katika Mkoa wa Guangdong nchini China. (Xinhua/Liu Dawei)
BEIJING - Baraza la Serikali la China Jumanne wiki hii limetoa agizo, likitaka kutekelezwa kwa sera na hatua mfululizo ili kuleta utulivu zaidi wa uchumi.
Sera na hatua hizo mfululizo zimetangazwa katika mkutano wa utendaji wa Baraza la Serikalil la China wiki iliyopita, zikiwa pamoja na hatua 33 zinazohusu sera za kibajeti na mambo ya fedha pamoja na sera za uwekezaji, matumizi, usalama wa chakula na nishati, minyororo ya viwanda na ugavi, pamoja na maisha ya watu.
Kwa mujibu wa agizo hilo, China itaimarisha hatua za kurejesha kodi ya thamani ya nyongeza iliyolipwa, kuharakisha matumizi ya fedha na kuharakisha utoaji wa dhamana maalum za serikali za mitaa.
Kwa upande wa sera za kibajeti na mambo ya fedha, serikali itapunguza gharama halisi za kukopa, kuongeza ufanisi wa ufadhili kupitia masoko ya mitaji, na kuimarisha usaidizi wa kifedha kwa miundombinu na miradi mikubwa.
Agizo hilo linasema, katika uwekezaji na matumizi, China itaongeza uwekezaji katika miundombinu ya usafiri, kuhimiza maendeleo ya uchumi wa mitandaoni na kuchochea ununuzi wa magari na vifaa vya nyumbani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma