久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

China yaondokana na ukali wa mlipuko wa Omicron na takwimu zenye kuonesha ufanisi wa uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 01, 2022

Wafanyakazi wakifanya kazi katika karakana ya Kampuni ya Usambazaji wa Umeme ya Anhui ya Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui nchini China, Mei 13, 2022. (Xinhua/Liu Junxi)

BEIJING - Sekta ya viwanda ya China iliimarika vyema Mwezi Mei, takwimu rasmi zilizotolewa Jumanne wiki hii zimeonesha, huku viwanda vingi vikirejea tena katika shughuli za uzalishaji baada ya mlipuko wa virusi vya Omicron kudhibitiwa.

Takwimu rasmi kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zinaonyesha kuwa, faharisi ya wasimamizi wa manunuzi (PMI), ambayo ni kipimo kikuu cha shughuli za viwandani ilifikia 49.6 Mwezi Mei, kutoka 47.4 mwezi wa Aprili.

Kwa mujibu wa kipimo hicho, kikisomeka zaidi ya 50 maana yake kinaonesha kupanuka kwa PMI, wakati kikisomeka chini ya 50 kinaonyesha kupungua kwa PMI.

"Uchumi wa China ulipata pigo kutokana na mlipuko wa Omicron na mabadiliko katika hali ya kimataifa, lakini umeimarika Mwezi Mei kutokana na uratibu madhubuti wa kuzuia janga na maendeleo ya kiuchumi na kijamii," Mtakwimu Mkuu wa NBS Zhao Qinghe alisema.

Kiwango kidogo cha uzalishaji wa viwandani kilikuwa 49.7 Mwezi Mei, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.3 kutoka mwezi uliopita, na kiwango kidogo cha oda za bidhaa za viwandani kilikuwa 48.2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.6 kutoka Aprili.

"Kati ya viwanda 21 vilivyofanyiwa uchunguzi, idadi ya viwanda vilivyopanua PMI ilifikia 12 Mwezi Mei kutoka 9 Mwezi Aprili, ikionyesha mabadiliko yenye matumaini katika sekta ya viwanda nchini," Zhao alisema.

Mwezi Mei, kiwango kidogo cha muda wa utoaji na usambazaji wa bidhaa kiliongezeka kwa asilimia 6.9 hadi 44.1, ikionyesha kuwa usafirishaji wa bidhaa uliendelea kukua polepole licha ya uboreshaji fulani.

Kielezo cha bei ya ununuzi kwa malighafi za msingi kilisimama kwa 55.8, asilimia 8.4 chini ya mwezi uliopita, lakini bado kinaendelea kwa kiwango cha juu.

"Mzunguko wa PMI Mwezi Mei unaonyesha kuwa athari za janga hilo zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa, na sera za kuleta utulivu wa ukuaji wa uchumi zimeanza kuonyesha athari chache," alisema Zhang Liqun, Mtafiti wa Kituo cha Utafiti wa Maendeleo cha Baraza la Serikali la China.

Zhang ametoa wito wa kuwepo kwa uratibu mzuri zaidi kati ya kuzuia janga na maendeleo ya kiuchumi, na juhudi kubwa zaidi za kuibua uwezekano wa ukuaji wa uchumi haraka iwezekanavyo na kuimarisha kasi ya kufufua uchumi.

Takwimu hizo pia zimeonyesha kuwa PMI ya sekta isiyo ya viwanda ya China ilikuwa 47.8 Mwezi Mei, kutoka 41.9 Mwezi wa Aprili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>