Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na John Lee, Mtendaji Mkuu mpya wa Hong Kong
Rais Xi Jinping akikutana na kufanya mazungumzo na John Lee, Mtendaji Mkuu mpya wa Serikali ya awamu ya sita aliyechaguliwa hivi karibuni wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Mei 30, 2022. (Xinhua/Li Xueren)
BEIJING - Rais Xi Jinping jana Jumatatu amekutana na kufanya mazungumzo na John Lee, Mtendaji Mkuu mpya aliyechaguliwa hivi karibuni wa serikali ya awamu ya sita katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) huko Beijing.
Lee, ambaye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 8, ataanza rasmi majukumu yake Julai 1, 2022.
Xi amempongeza Lee kwa ushindi wake katika uchaguzi na kuteuliwa na Serikali Kuu ya China.
Akimsifu Lee kwa kudumisha msimamo usioyumba wa kupenda nchi na Hong Kong, kuwa tayari kubeba majukumu na kutekeleza kazi zake kikamilifu, Xi amesema Lee ametoa mchango katika kulinda usalama wa taifa, ustawi na utulivu wa Hong Kong katika majukumu mbalimbali.
"Serikali Kuu inatoa uthibitisho kamili kwako na kuwa na imani kamili kwako," Xi amemwambia Lee.
Chini ya mfumo mpya wa uchaguzi, tangu mwaka jana Hong Kong imefanikiwa kufanya uchaguzi wa Kamati ya Uchaguzi, Baraza la Kutunga Sheria la awamu ya saba na mtendaji mkuu wa awamu ya sita.
Xi amesema, imethibitishwa kuwa mfumo mpya wa uchaguzi ulichukua jukumu muhimu katika kutekeleza kanuni ya "wazalendo kusimamia Hong Kong," kuhakikisha nafasi ya watu wa Hong Kong kujitawala wao wenyewe, na kuwezesha mazingira mazuri ambapo sekta zote za jamii hufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya Hong Kong.
"Huu ni mfumo wa kisiasa na kidemokrasia ambao unaendana na kanuni ya 'nchi moja, mifumo miwili' na inafaa kwa hali halisi ya Hong Kong na mahitaji ya maendeleo," Xi amesema. "Lazima itunzwe na kuzingatiwa kwa muda mrefu ujao."
Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 25 tangu Hong Kong irejee kwa nchi mama ya China.
"Licha ya changamoto katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, utekelezaji wa kanuni ya 'nchi moja, mifumo miwili' huko Hong Kong umekuwa na mafanikio makubwa," Xi amesema.
"Azimio la Serikali Kuu la kutekeleza kikamilifu na kwa uaminifu kanuni ya 'nchi moja, mifumo miwili' halijawahi kuyumba, bado halitabadilika hata kidogo," amesema.
Maafisa waandamizi akiwemo Han Zheng na Xia Baolong walihudhuria mkutano huo.
Rais Xi Jinping akikutana na kufanya mazungumzo na John Lee, Mtendaji Mkuu mpya wa Serikali ya awamu ya sita aliyechaguliwa hivi karibuni wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Mei 30, 2022. (Xinhua/Li Xueren)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma