Lugha Nyingine
China yatangaza hatua za kuleta utulivu na kuinua kiwango cha biashara na nje
Picha iliyopigwa Mei 1, 2022 ikionyesha meli ya kontena ikitia nanga kwenye Kituo cha Kontena cha Qianwan huko Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Ziheng)
BEIJING - China imetangaza hatua za kina za kuleta utulivu na kuinua kiwango cha biashara na nje, kufanya juhudi za kudumisha utulivu wa uchumi na minyororo ya viwanda na usambazaji wa bidhaa. Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa siku ya Alhamisi na Baraza la Serikali la China, ambalo ni kama baraza la mawaziri la China, huduma kwa makampuni muhimu ya biashara ya nje zitaimarishwa na hatua zitawekwa ili kuhakikisha usafirishaji wa bidhaa kwa utaratibu bila matatizo katika kufanya biashara na nje.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, msaada wa mitaji na kifedha kwa makampuni ya biashara ya nje utaimarishwa, wakati huo huo kufanya juhudi za kuimarisha biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka, kuandaa .
Mwongozo huo pia unabainisha kuwa maonyesho ya kibiashara ya mtandaoni yanapaswa kuboreshwa ili kusaidia makampuni kuongeza kiasi cha miamala ya biashara na nje, na kuanzisha maeneo mapya ya vielelezo vya kuhimiza uagizaji bidhaa kutoka nje.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma