Lugha Nyingine
Tunisia yaandaa kongamano la uwezeshaji wa kifedha ili kukuza biashara na uwekezaji barani Afrika
Waziri Mkuu wa Tunisia Najla Bouden Romdhane akizungumza katika mkutano wa tano wa Kongamano la Kuwezesha Uwekezaji na Biashara barani Afrika (FITA 2022) huko Tunis, Tunisia, Mei 25, 2022. Kongamano la FITA 2022 limefunguliwa jana Jumatano nchini Tunisia, kwa lengo la kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi za Bara la Afrika. (Picha na Adel Ezzine/Xinhua)
TUNIS – Mkutano wa tano wa Kongamano la Uwezeshaji wa Uwekezaji na Biashara barani Afrika (FITA 2022) umefunguliwa jana Jumatano nchini Tunisia, kwa lengo la kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi za Bara la Afrika.
Akifungua kongamano hilo la siku mbili, Waziri Mkuu wa Tunisia Najla Bouden Romdhane amesema takriban watu 3,500 kutoka nchi 45, wakiwemo mawaziri kutoka nchi za Afrika na wakuu wa mashirika na taasisi za kimataifa, wanashiriki katika tukio hilo “l(fā)a kipekee”.
“Janga la UVIKO-19 na mgororo kati ya Ukraine na Russia, pamoja na kuongezeka kwa bei za malighafi, vyakula na mafuta, kumedhoofisha uchumi wa nchi za Afrika” Bouden amebainisha.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, Bouden ametoa wito wa "dhana mpya na zenye ubunifu ili kuinua ushindani wa Bara la Afrika na kuendeleza maendeleo yake ya kijamii na kiuchumi, ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara."
Wawakilishi wakihudhuria mkutano wa tano wa Kongamano la Uwezeshaji wa Uwekezaji na Biashara barani Afrika (FITA 2022) huko Tunis, Tunisia, Mei 25, 2022. (Picha na Adel Ezzine/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma