Lugha Nyingine
Xi Jinping akutana na Bachelet, kamishna mwandamizi wa UM anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu
Tarehe 25, Mei, rais Xi Jinping wa China alikutana na Bachlet, kamishna mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu kwa kupitia video hapa Beijing. (Picha/Xinhua)
Tarehe 25, Mei, rais Xi Jinping wa China alikutana na Bachlet, kamishna mwandamizi wa UM anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu kwa kupitia video hapa Beijing.
Rais Xi alimkaribisha Bi. Bachlet kufanya ziara nchini China, akieleza kwa kina masuala muhimu kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika mambo ya haki za binadamu nchini China kwa muktadha wa historia na utamaduni wa China, na kueleza msimamo wa kikanuni wa Chama cha CPC na Serikali ya China wa kujikita katika kulinda na kuhakikisha haki za binadamu kwa pande zote. Xi alisisitiza kuwa, kuanzia siku ya kuzaliwa kwa Chama cha CPC, chama hicho kilishikilia nia yake ya kuwatafutia furaha watu wa China na kustawisha taifa la China, na katika zaidi ya miaka 100 iliyopita, siku zote chama hicho kikiwa kinafanya juhudi kwa ajili ya maslahi ya watu. Matarajio ya watu kwa maisha bora ni lengo letu la kufanya juhudi. Baada ya kufanya mapambano magumu kwa muda mrefu, China imefaulu kufuata njia ya kuendeleza mambo ya haki za binadamu inayoendana na mkondo wa zama na inayofaa hali halisi ya nchi hiyo.
Bi. Bachlet alisema, anashukuru upande wa China kumkaribisha kufanya ziara nchini China wakati wa kushinda taabu za maambukizi ya virusi vya korona. Hii ni mara ya kwanza kwa kamishna mwandamizi wa UM anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu kufanya ziara nchini China katika miaka 17 iliyopita, anatilia maanani na kuithamini sana ziara hiyo, na atakutana na kuzungumza moja kwa moja na serikali ya China na watu wa sekta mbalimbali nchini humu. Anaamini ziara hiyo itamsaidia kuijua China vizuri zaidi.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Michelle Bachlet, kamishna mwandamizi wa UM anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu kwa kupitia video hapa Beijing, China, Mei 25, 2022. (Picha/Xinhua)
Picha ikionesha Bachelet kuhudhuria mkutano huo huko Guangzhou, Kusini mwa Mkoa wa Guangdong wa China. (Xinhua/Deng Hua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma