Lugha Nyingine
Wizara ya Biashara ya China yajibu kuhusu Mpango wa Marekani wa uchumi wa eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki
Picha ya kumbukumbu ikionyesha geti la Wizara ya Biashara ya China hapa Beijing, Mji Mkuu wa China. (Xinhua/Li He)
BEIJING - China inaamini kuwa Mpango mpya wa uchumi wa eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki (IPEF) unapaswa kuhimiza ustawi, maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi badala ya kuharibu na kuvuruga mipango mingine iliyopo katika eneo la Asia-Pasifiki.
Wizara ya Biashara ya China katika taarifa yake ya kujibu mpango huo wa Marekani imesema kwamba, Mafanikio ya uchumi wa Asia na Pasifiki yanatokana na kufungua milango , kufanya ushirikiano na kunufaishana. Juhudi husika zinapaswa kuchangia ustawi na maendeleo ya eneo hilo, ziwe wazi na shirikishi badala ya ubaguzi na upendeleo, na kukuza ushirikiano wa kiuchumi na mshikamano badala ya kuharibu na kuvuruga mipango iliyopo.
"China bado iko wazi kwa mpango wowote wa kiuchumi wa kikanda ambao unaambatana na kanuni zilizotajwa hapo juu," Msemaji wa wizara hiyo amesema Jumatatu wiki hii.
Msemaji huyo amesema kwamba, China itazingatia uwazi wa kikanda na kushiriki ustawi na changamoto pamoja na washirika wenzi wake wa kibiashara katika eneo la Asia-Pasifiki.
“China iko tayari kuendeleza ushirikiano wa kivitendo na pande zote ili kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda, kuinua uchumi wa kikanda, na kudumisha amani na maendeleo ya kikanda” Msemaji huyo ameeleza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma