Lugha Nyingine
China kuendelea kuleta utulivu katika uwekezaji wa kigeni huku kukiwa na changamoto
Picha iliyopigwa Januari 14, 2021 ikionyesha mwonekano wa usiku wa Lujiazui katika eneo la Pudong la Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)
BEIJING - Wizara ya Biashara ya China imesema Alhamisi wiki hii kwamba itaendelea kuleta utulivu kwenye uwekezaji wa kigeni na kutoa mazingira bora ya biashara na huduma kwa makampuni ya kigeni.
"Ikiathiriwa na mambo mengi, China inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutumia mtaji wa kigeni," Shu Jueting, Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
"Lakini mambo mazuri yanayosaidia China kufanya uwekezaji nje hayajabadilika," Shu ameongeza.
Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) kwa China Bara, katika matumizi halisi, uliongezeka kwa asilimia 20.5 hadi kufikia yuan bilioni 478.61 katika miezi minne ya kwanza ya mwaka huu, takwimu kutoka wizara hiyo zinaonyesha.
“Kwa hesabu za dola za Marekani, mitaji hiyo iliongezeka kwa asilimia 26.1 kuzidi mwaka uliopita hadi kufikia dola bilioni 74.47” imesema wizara hiyo.
Shu alisema, ongezeko la haraka la uwekezaji wa kigeni linatokana na soko la China linalovutia, juhudi za kufungua mlango, na mazingira bora ya biashara.
"China inaendelea kubaki na sera za kuvutia uwekezaji wa kigeni kwani misingi yake ya kiuchumi kwa ukuaji wa muda mrefu bado ni thabiti na isiyobadilika. Makampuni ya kigeni yana matumaini kuhusu matarajio yao ya maendeleo ya muda mrefu nchini China," Shu ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma