Lugha Nyingine
Xi apongeza kongamano la maadhimisho ya miaka 50 ya matumizi ya dawa ya kutibu malaria ya artemisinin
Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa kongamano la kimataifa la maadhimisho ya miaka 50 ya matumizi ya dawa ya malaria artemisinin, lililofunguliwa leo Jumatatu mjini Beijing, ambalo pia linalenga kusaidia ujenzi wa pamoja wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ya afya.
Rais Xi amesema artemisinin ni dawa maalum ya kwanza ya kutibu malaria iliyogunduliwa na kutolewa kwa mafanikio na China, akiongeza kuwa dawa hiyo imesaidia China kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria katika kipindi cha miaka 50 tangu ilipoanza kutumiwa.
Amesema China imehimiza kikamilifu matumizi ya artemisinin duniani, kuokoa maisha ya mamilioni ya watu, hasa katika nchi zinazoendelea, na kutoa mchango muhimu katika kuzuia na kutibu malaria na kulinda afya ya binadamu.
Ameongeza kuwa, China iko tayari kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa ili kuimarisha ushirikiano katika afya ya umma, kukabiliana kwa pamoja na vitisho na changamoto za kimataifa, na kujenga jumuiya ya kimataifa ya afya kwa wote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma