Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Bw. Aleksandar Vucic kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Serbia
Tarehe 5 Aprili, Rais Xi Jinping wa China ametumia salamu za kumpongeza Bw. Aleksandar Vucic kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Serbia.
Katika salamu zake za pongezi Xi Jinping amesema, katika miaka ya hivi karibuni, mwelekeo wa ukuaji wa hali motomoto umeonekana siku zote katika uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Serbia. Nchi hizi mbili zimedumisha hali ya kuaminiana kisiasa, na mafanikio mengi yamepatika katika ushirikiano wa kufuata hali halisi. Kwa kukabiliwa na mabadiliko makubwa ya dunia ambayo hayakutokea katika miaka mia moja iliyopita, pande hizi mbili zimeshikilia kuheshimiana na kutendeana kwa usawa, kuhimiza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutoa mchango wenye hamasa kwa ajili ya kulinda haki na usawa wa kimataifa. Rais Xi Jinping amesema kuwa “Ninatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Serbia, na ninathamini uhusiano mzuri wa kikazi na urafiki kati yangu na Rais Vucic, ningependa kufanya juhudi pamoja na Rais Vucic katika kuongeza mawasiliano ya kimkakati kati ya nchi hizi mbili, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua na kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kunufaishana kwenye sekta mbalimbali, na kuongoza uhusiano kati ya China na Serbia uendelee kupata mafanikio mapya ili kuleta manufaa kwa nchi hizi mbili na wananchi wao.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma