Lugha Nyingine
China yasema inamkaribisha mkuu wa haki za binadamu wa UN kutembelea Xinjiang
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema China inamkaribisha Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet kutembelea nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kufanya ziara mkoani Xinjiang.
Wang alihudhuria Mkutano wa 58 wa Usalama wa Munich kwa njia ya video mwishoni mwa wiki iliyopita na alitoa kauli hiyo wakati akijibu maswali kuhusu Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang nchini humo.
Wang amesema China kwa muda mrefu imemkaribisha Bachelet, na inajadiliana na Bachelet na ofisi yake kuhusu ratiba, na kwamba Bachelet wakati wa ziara yake ataishuhudia Xinjiang ambako amani na utulivu vinadumishwa na watu wa makabila mbalimbali wanaishi kwa amani.
Akibainisha kuwa Mkoa wa Xinjiang uko jirani mwa eneo ambalo vikundi vya magaidi na watu wenye itikadi kali wamejazana kwa wingi, Wang amesema Serikali ya Mkoa wa Xinjiang, ili kudumisha usalama wa watu, ilifanya kazi ya kuondoa itikadi kali kupitia utoaji wa elimu, kwa kufuata uzoefu wa nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza na Ufaransa na utaratibu wa kimataifa.
Wang amesema, kazi hiyo kimsingi imeondoa udongo wa itikadi kali, na kupata uungwaji mkono wa watu wa Xinjiang. Ameongeza kuwa katika miaka mitano iliyopita, hakujatokea matukio ya kimabavu ya kigaidi katika eneo hilo.
Kile kinachojulikana kama "kulazimishwa kufanya kazi" au "kambi za kuelimisha upya" zote ni uwongo na uzushi, Wang amesema.
“China inakaribisha wageni kutembelea Xinjiang ili kujifunza ukweli wa jambo hilo” Wang amesema, huku akibainisha kuwa kabla ya kuzuka kwa janga la UVIKO-19, Xinjiang ilipokea zaidi ya maafisa 2,000 wa serikali, viongozi wa kidini na waandishi wa habari kutoka zaidi ya nchi 100 na mashirika ya kimataifa.
"Lakini jambo moja ni hakika, watu wa makabila yote huko Xinjiang hawafurahii uchunguzi wowote unaotokana na dhana ya hatia, na wanapinga vikali aina mbalimbali za upendeleo na shutuma zisizo na msingi dhidi ya sera za China zinazohusu makabila," Wang amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma