Lugha Nyingine
Katuni: Kuzusha "Tukio la Sanduku la kuwatunza vichanga " ili kuchochea chuki na kupamba moto kwa vita
Mwaka 1990, Oktoba, Idara ya Ujasusi ya Marekani ilizusha “Tukio la Sanduku la kuwatunza vichanga” ambalo lilichochea ghadhabu za Wamarekani kwa Iraq na kupamba moto kwa vita vya ghuba.
“Niliona askari wa Iraq wakikimbilia hospitalini wakishika bunduki na kuingia wodini. Walikuwa wanachukua vichanga 15 kutoka sanduku hilo na kuwaacha walale kwenye sakafu baridi hadi kufa.” Wakati huo, msichana mwenye umri wa miaka 15 aliyejidai kuwa ni mtu wa kujitolea wa Kuwait aliwashutumu askari wa Iraq akilia kwa uchungu katika Bunge la Taifa la Marekani.
Habari hiyo ilitolewa na vyombo vingi vya habari vya Marekani na kuchochea ghadhabu kubwa za Wamarekani kwa Iraq. BBC ilisema kuwa rais wa Marekani wa wakati huo Senior Bush alinukuu ushahidi huo hadharani kwa mara zaidi ya sita kuwa sababu ya kupeleka wanajeshi wa Marekani kushiriki kwenye vita vya ghuba.
Baadaye, Bunge la Taifa la Marekani lilitoa azimio la kuanzisha vita dhidi ya Iraq, na vita vya ghuba vililipuka. Lakini baada ya kumalizika kwa vita hivyo, baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani vilifichua “Tukio la Sanduku la kuwatunza vichanga ” ni uzushi wa Marekani, na madaktari wa Kuwait walidhihirisha mapema kuwa, kabisa hakuwepo mtu huyo wa kujitolea wa Kuwait.
“Tukio la Sanduku la kuwatunza vichanga ” ni mchezo uliooneshwa pamoja na wanasiasa na vyombo vya habari vya Marekani tu. Walitumia maoni ya umma kwa kudhibiti hisia za upendo na chuki za watu ili kutimiza malengo yao ya kisiasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma